Site Loader

Kinywa / Meno

Mdomo wako na koromeo lako zitakauka ukipumulia mdomo.Tumia maji mengi na utumie tumia dawa ya kikohozi (za kumumunya).

Jua linaweza kuchoma mdomo wako wa chini vibaya ukitumia losheni za kuzuia jua ya zinki itakuwa ngao yako dhidi ya tukio hili.

Kutana na daktari wa afya ya kinywa kabla ya kusafiri.maumivu ya jino kwa siku kadhaa kunaweza kukuondolea burudani ya safari yako.

Matatizo yote ya meno yanaweza kuzuiwa.Uchafu wa kinywa unaweza kuchochea tatizo la magego ya mwisho ambao huwapata sana chipukizi.Hewa ya baridi katika uwanda wa juu utatibua mashimo yaliyojazwa na kuvunjika au kutibiwa kwenye meno.

Sukari nyingi sana huweza kusababishauchungu sana kwenye kishimo kilichooza kwenye jino au ung’oaji ambao hauwezekani kwenye safari za kivumbuzi.

Maambukizi ya meno mengi na ufizi huweza kukomeshwa kirahisi kwa dawa za Amoxycillin na Metronidazole.Unaweza pia kutumia ibuprofen kupunguza uvimbe.

Kwenye uwanda wa juu:
• Kunywa maji mengi kulainisha kinywa-midomo, mdomo na koromeo.
• Yahami midomo kwa krimu ya zinki.
• Fungasha antibayotiki na ibuprofen kwa ajili ya uvimbe wa fizi na maumivu makali.

Maandalizi:
• Chunguza meno kwa eksirei wiki sita (6) kabla ya safari.
• Nunua krimu ya zinki kwa ajili ya midomo.
• Nunua kipodozi-kijiti cha kuzuia mdomo kubabuka.
• Nunua tembe mumunyi za kikohozi.

Kwa muda wa mwezi mmoja kwenye kituo cha afya ya kinywa ya Namche Baaazr, mwandishi wa kitabu hiki aliawtibu wapandaji milima wa misafara saba waliokuwa wakielekea mlima Everest.Lhotse, Nuptse, Ama Dablam na Pumori walioambulia dalili mbaya za meno.Hakuna aliyechunguzwa meno kabla ya kuondoka nyumbani kuelekea safarini.

Previous         Next