Site Loader

Mazingira salama

Mazingira katika nyanda za juu hayatabiriki kuliko katika nyanda za chini. Kwa hiyo, michakato ya uasilia ni ya taratibu sana na kuingiliwa kwake kunaweza kuleta madhara ya muda mrefu.

Manyumbani mwetu upatikanaji wa maji, nishati na chakula na utupaji taka si masuala tete kwetu. Kwenye nyanda za juu tunahitajika kuwajibika. Tukifanyacho huwaathiri wakazi na wageni watakaoabiri hapo.

Ujue kwamba wenyeji hukamua rasilimu zao adhimu kuboresha huduma ili ziwe za kisasa kuhakikisha kwamba wageni wao wanaridhika.

Maji ni adimu:

Usijihusishe na lolote linalochafua mito.

Epuka bafu ya manyunyu ya maji – moto au baridi. Ndoo ya maji inatosha.

Tumia choo cha shimo si cha maji.

Chakula si rahisi kuotesha:

Nunua chakula kinapopatikana.

Jihadhari kama unanunua chakula huko mbali – watu wanaweza wakakuuzia chakula walichokihifadhi kwa ajili ya msimu wa baridi.

Mbao ni adhimu:

Hakikisha unachukua nishati unayohitaji kwa kila mmoja.

Hakikisha huwahimizi watumishi kukusanya na kuchoma mbao/usihimie matumizi ya kuni.

Unga mkono jitihada za upandaji miti.

Taka ni tatizo kubwa:

Usinunue maji ya chupa. Baada ya kutumia maji yake hazitoweki ng’o!

Ondoka na ulichoingia nacho. Vifungashio virudishwe nyumbani.

Rudi na betri zako nyumbani.

Tambua kinachotokea kwenye takataka za wanakikundi na usitishe tabia mbaya.

Tumia choo cha shimo refu kilichohifadhiwa vizuri. Chimbia sana au usambaze kinyesi chalo (Au ubebe urudi nacho) inaweza kuchukua muda mrefu kusambaratika.

Panga namna ya kutupa vyombo vya usafi.

Mimea na wanyama huzoea kirahisi mazingira katika nyanda za juu:

Using’oe mimea.

Usiharibu udongo.

Walinde wanyama na mimea-pori.

Previous         Next