Site Loader

Antaktika

Antaktika ni bara lenye baridi,lililo katika uwanda wa juu,lenye tufani na theluji kuliko yote duniani likiwa na wastani wa mwinuko wa M.2300. Parefu zaidi pakiwa mlima Vinson kwenye M.4,892.Theluji huweza kufikia hadi kina cha m.4,700 katika baadhi ya maeneo.Watu wengi hutembelea Antaktika kama sehemu ya ziara yenye malengo mahsusi au kazi mradi na yenye mafunzo ya masharti na miongozo ambayo yanalazimu yafanyike katika nyanda za juu.Hata hivyo bara linavyojipambanua kuwa huria,baadhi ya makampuni hujitokeza kutoa huduma za kukwea nyanda za juu huko.Ikumbukwe kwamba kanieneo ni ya chini kabisa katika ncha za dunia.mifumo ya chini ya hali ya hewa ya kanieneo huweza pia kushusha kanieneo zaidi.Matokeo yake upungufu wa viwango oksijeni na AMS hutokea katika kina cha chini kuliko kokote.

Baridi iliyokithiri husababisha magonjwa ya miinuko mirefu kuwa hatari zaidi.

Mtalii mwenye umri wa miaka 66,Mzima na uzima wake,aliruka kwa ndege akitokea kambi ya Patriotic Hills,M.887 hadi kwenye ncha ya dunia(Antaktika m.2800.Bibie akajiharakisha matembezi ya m.300 hadi kwenye bendera kupiga picha.Baadaye akahitaji msaada wa kupiga hatua 30 hadi kwenye kituo cha utafiti cha NSF.Aliishiwa pumzi iliyoambatana na kuumwa kichwa.Alitibiwa na oksijeni,majimaji na dawa za maumivu tu.Baadaye siku ile aliweza kutembea hadi kwenye ndege na kurejea hali yake ya afya njema ya awali akiwa Patritot Hills siku iliyofuata.

Previous         Next