Site Loader

Austaralia

New Zealand ina vilele vingi juu ya m.3000 ingawa ni matukio machache sana yameripotiwa yaliyohitaji uokoaji dhidi ya magonjwa ya nyanda za juu.Hata hivyo ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi (frostbite)ni kawaida.kwenye mlima Cook.

Kilele cha juu kabisa kwenye mlima Kosciuszko (m.2200) ni safari rahisi ya matembezi hivyo haiwezi kusababisha changamoto za nyanda za juu ingawa bado inawezekana.

Papua New Guinea/Indonesia zina milima mingi yenye urefu wa Zaidi ya m.3000,mrefu Zaidi ukiwa Puncak Jaya(Carstensz Pyramidi) wenye m.4884.Watalii wengi wameripoti dalili za magonjwa ya nyanda za juu yaliyotia doa kwenye safari zao huku wengine wakipoteza maisha.Kama vilelele vya Afrika,ni muhumu kupanda na taraitbu na kujaribu kuizoea pale pawezekanapo.Ugumu wa kufuatilia,ukosefu wa ramani makini,majira ya unyevunyevu na matope,huduma dhaifu za afya na hatari za magonjwa ya kitropiki huweza kugeuza safari rahisi kuwa ndoto za alnacha.

Bomeo-Mlima Kinabalu m.4101 huweza kukwewa haraka na matokeo yake ni madhara ya taathira za magonjwa ya nyanda za juu.

Mnamo mwaka 1982,wapandaji wawili walizuiwa na tufani kwenye kilele cha mlima Cook.Hali ya hewa ilipoboreka na kuokolewa,wengi waliugua kuganga tishu kwa jalidi kwenye miguu yao kwa sababu ya mseto wa baridi na uwanda wa juu. Wanaume wote wawili walikatwa miguu.Wote wawili walirudi mlimani hadi kileleni na mmmojawapo alifika pia kilele cha mlima Everest.

Previous         Next