Site Loader

Asia

Maeneo mengi mashuhuri kwa safari za mbali na upandaji milima katika nyanda za juu yamo  katika ukanda huu wa dunia.

Kuanzia Nepali, Pakistani au India inawezekana kabisa kupanda taratibu kuelekea milimani-kimsingi kuepuka utiaji kambi ghafla katika maeneo ya nyanda za juu.Asilimia 84 ya warukao kwa ndege na kutua katika hoteli ya ‘Everest view’ m.3,600 waliugua magonjwa ya nyanda za juu(AMS).

Kupanda taratibu kuelekea uwanda wa juu wa Tibet si rahisi, kwa hiyo dalili za magonjwa ya miinuko mirefu(AMS) haina budi kusimamiwa kwa makini na mazoezi yawe ya kawaida hadi kuyazoea hali ya hewa ya mazingira husika.

Wakiendesha baiskeli kutoka Lhasa kuelekea kambi ya Everest, kundi la waendesha baiskeli walivuka njia nyembamba mbili zenye urefu wa m.5000 kwa siku 8. Siku ya 9,wakiwa katika umbali wa m.4,150,mmoja wao aliamka akijihisi kizunguzungu na kichefuchefu,alitetemeka na hakuweza kutembea wima.kma Saa sita hivi,,pasi na kuonesha nafuu,kundi liliamua kushuka.Hapa walishavuka m.5,150.Muathirika akageuka bluu.akihema kwa shida,akigonganisha meno na kutoa mapovu mdomoni.Baada ya kuendelea kushuka,hali yake ilibadilika kuwa nzuri.Kundi likakaa kwenye mwinuko wa m.4100.usiku huo na daktari mwenyeji akamshuku kwa shinikizo damu la juu kiuongo.Kwa bahati nzuri wakakutana na daktari maalum wa ukweaji milima mwenye tiba za magonjwa ya nyanda za juu.Walishuka hadi m.2400 kwa gari siku iliyofuata na mwisho hadiKathmandu kwa ajili ya huduma za afya.

Previous         Next