Site Loader

Oksijeni

Kukosekana kwa oksijeni husababisha magonjwa mengi ya nyanda za juu. Suluhisho pekee la tatizo ni kupata oksijeni zaidi. Hili huwezekana kirahisi na kimantiki kwa kushuka au kama hili haliwezekani, kuna masuluhisho mawili zaidi katika uwanda wa juu.

(1) Kutoka kwenye chupa ya oksijeni silinda ya oksjeni inaweza kurekebishwa kwa kutumia uso wa bandia.Mtu mwenye mahitaji ya oksijeni,mara moja huweka uso wa bandia na kuvuta oksijeni,akiichanganya na hewa ya mazingira yake.Akitumia ‘kimfuko  cha oksijeni chenye mtiririko uleule’ lau lita 2 kwa dakika, chupa ya lita 300 itaisha kwa muda wasaa 2 hadi 3.Ukitumia mfuko wa oksijeni wa ‘mtiririko wa kimahitaji’(oksijeni hutoka wakati wa kuvuta hewa tu),Chupa yenye ujazo sawa  huweza kuisha baada ya saa 6 hadi 9..

(2) Kwenye mfuko wa shinikizo

Wale wanaugua magonjwa ya nyanda za juu(AMS),tatizo la pumzi kama matokeo ya maji kujaa kwenye mapafu(HAPE) au uvimbe wa vimiminika kwenye ubongo  utokeao kwenye uwanda wa juu (HACE) wanaweza kutiwa ndani ya begi liitwalo begi la chumba cha kulala katika nyanda za juu(PAC),Certec au begi la Gamow (Gamow bag).Begi hili hujazwa pumzi kuongeza hewa ndani mwake ili pumzi ya oksijeni inayopumuliwa iwe kama m.2000 chini.Mgonjwa awe humo ndani kwa muda wa saa ingawa anaweza akahitaji muda mwingi zaidi.Kuinua kisogo kunaweza kusaidia upumuaji mzuri.Ingawa mabegi haya huweza kuokoa maisha,yana changamoto zake:

Ni vigumu kuwasiliana na mgonjwa akiwa ndani mwake.

Mgonjwa mahututi anahitaji mwangalizi kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu.

Ngoma ya sikio huweza kupata shida.

Hewa iliyo ndani huhitaji kubadilishwa.

Ahueni huwa ya muda mfupi.

Wanandoa waliamua kusafiri kwenda kupanda mlima Kilimanjaro(M.5,895)kupitia njia ya Marangu.Baada ya siku mbili ya upandaji walifika kituo cha Horombo(m.3760).Ndani ya saa mbili,mume alianza kupata tatizo la upumuaji.Wakati wa usiku alianza kukohoa na kutoa makohozi ya pinki na kupoteza fahamu.Aliugua ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu-HAPE, na alitiwa kwenye mfuko wa Gamow kwa masaa manne.Alipata nafuu na kuweza kushuka na wachukuzi,baada ya huduma ya hospitali alipona kabisa.

Previous         Next