Site Loader

Vidonge na vijidonge

Hakuna ziara ielekeayo kwenye uwanda wa juu bila dawa fulani.Baadhi ni maelekezo ya madaktari na sharti itumike tu kwa maelekezo ya madaktari.Mengine yataokoa maisha yako ilhali mengine yatalegeza dalili fulani na kukuruhusu ufurahie safari yako.

Hapa chini kuna jedwali la orodha ya fupi ya dawa zitumikazo kwenye kwenye nyanda za juu.Litumie ili iwe muongozo wa kufanya uamuzi wa dawa za kutumia,ila kumbuka ushauri wa tiba hubadilika kwa hiyo angalia kabla ya kwenda.

Kila mara uwe na barua ya daktari kuhusu tiba zako kuepuka usumbufu wa kisheria.

Kwenye uwanda:
• Hakikisha wewe una dawa na barua ya tabibu wako.
• Beba dawa katika vifungashio zenye lebo ya jina na dozi na rahisi kufungua, mabegi ya zipu.
• Hakikisha unameza dawa kwa kutumia maji kila mara – huziwezesha kufanya kazi vizuri.

Maandalizi:
• Peleka orodha hii kwa daktari wako na ujadili naye dawa husika tayari kwa matumizi.
• Nunua dawa nyumbani. Hazina yako iwe na isheheni zote isipokuwa oksijeni. Dawa zinaweza kuwa chee ughaibuni lakini zisizo halisi.
• Thibitisha mzio wowote.

Niliumwa mabegani nikahisi maumivu kama ya kudundwa na sindano.Dakika tatu baadaye nikaanza kujisikia kuwashwa.Dakika iliyofuata nikajihisi mikononi mwa mtu giza lilipotanda.wanakikundi wakaita pipa ya matibabu.Oksijeni, adrinalini,
Vidhoofisha-histamini na maji,yote haya alipewa mgonjwa kwa muda kama wa dakika kadhaa tu.Saa moja baadaye nilianza kupata nafuu.Siku iliyofuata,niliweza kuendelea na safari.Maisha yanawiwa na deni kubwa la hatua stahiki za madaktari wa safari hiyo.Sasa hubeba kifaa cha kudungia mgonjwa wa mzio hatari.Hii ni kwa tahadhari.

Previous         Next