Usingizi wa mang’amung’amu wakati wa siku za awali mlimani kwenye uwanda wa juu ni hutokea na ni kawaida.Unaweza kupata usingizi kwa shida,ukaamka sana na kuhisi kwamba hukulala vizuri,au ukajihisi kutokidhi haja ya pumziko.
Kutolala vizuri kunahusianishwa na namna mwili unavyojinasibisha na mabadiliko ya mazingira.Unavyoyazoea mabadiliko ya mazingira ubora wa usingizi hungezeka.Watu wenye magonjwa ya nyanda za juu (AMS) pia huweza kusababisha usingizi wa mang’amung’amu ukimaanisha kutozoea mazingira ipasavyo.
Dalili zingine kama mafua, kukoroma,au mshikemshike kitandani au kwenye hema huweza pia kuwa tatizo.
Uwanda wa juu pia huweza kusababisha idadi ya muda unaohitaji kukojoa, kwa hiyo hupoteza muda wa usingizi.
Mabadili mengi sababu yake ni kupumua mno.Kwa baadhi ya watu huweza kusababisha mpumuo mshtuko ‘periodic breathing’ usiku, ambapo mtu hupumua harakaharaka kisha upumuaji husitishwa kwa muda.Jambo linaloweza kukugutua usingizini.Hili ni la kawaida katika uwanda wa m.2800 kutoka usawa wa bahari na takribani kila mmoja hupatwa nalo kuanzia m.5000.Ingawa mpiga kambi kwenye hema anaweza akakutia hofu kwa hili, hupungua jinsi unavyozoea mabadiliko ya mazingira.
Kukoroma kunaweza kuwa kuchochewa zaidi na hewa kavu, yenye vumbi lakini kuziba kwa pua wakati wa usiku katika mwambao wa bahari haichochewi zaidi na mwinuko.
Kwenye uwanda wa juu:
• Tarajia kutamani usingizi zaidi.
• Epuka kafini na kilevi jioni.
• Kama usingizi hauboreki baada ya siku chache usiendelee juu. Shuka chini kuruhusu mwili uakisi mabadiliko ya mazingira.
Maandalizi:
• Wekeza kwenye faraja ya usingizi. Begi zuri la usingizi na mkeka.
• Fungasha vizibo laini vya masikioni (ear plugs) kwa usingizi mno.
• Kama una tatizo la ungonjwa wa mshtuko usingizini (obstructive sleep apnoea), muone daktari bingwa wa ugonjwa huo.
Nilipata usingizi kwa taabu sana kwani mwenzangu kwenye hema aliamka kila mara kwenda kukojoa.